1SA_Kiswahili_1068.pdf

(282 KB) Pobierz
1SAMWELI
Utangulizi
Katika andiko la Kiebrania, kitabu cha 1Samweli na 2Samweli vilikuwa kitabu kimoja kilichotambuliwa kwa
jina hilo. Huku kugawanyika na kuwa vitabu kuwa viwili kulifanyika katika tafsiri ya Septuagint, yaani,Agano la
Kale la Kiyunani, ambalo liliviita Kitabu cha Kwanza na cha Pili cha Wafalme.
Kitabu cha 1Samweli kinaandika habari za maisha ya Samweli, Sauli na sehemu kubwa ya maisha ya Daudi.
1Samweli kinaanza kuelezea kuzaliwa kwa Samweli na mafundisho yake hekaluni. Kinaelezea jinsi alivyoiongoza
Israeli akiwa kama nabii, kuhani na mwamuzi.
Wakati wana wa Israeli walipodai kuwa na mfalme, Samweli, kwa uongozi wa Mungu, alimtia Sauli mafuta
kuwa mfalme wa kwanza wa Waisraeli. Lakini Sauli aliacha kumtii Mungu, naye Mungu akamkataa asiendelee
kuwa mfalme. Kisha Mungu akamongoza Samweli akamtia Daudi mafuta kwa siri kuwa mfalme badala ya Sauli.
Mapambano kati ya Sauli na Daudi ndiyo yaliyomo katika sehemu iliyobaki ya kitabu hiki. Ingawa tunajifunza
mengi kuhusu watu hawa wawili, pamoja na kutokumtii Mungu kwa Sauli, pia kuna mkazo mkubwa kuhusu wema
wao kwa Mungu.
Wazo Kuu
Hiki kilikuwa ni kipindi cha mabadiliko katika historia ya Israeli, wakati taifa hili lilipoondokana na mfumo wa
kuwa na waamuzi kama viongozi wao na kuwa na mfalme kama mataifa ya jirani yalivyokuwa. Samweli, akiwa
nabii, kuhani na mwamuzi, alichangia kikubwa katika kipindi hiki.
Mwandishi
Ingawa 1 na 2Samweli mapokeo yanasema mwandishi ni Samweli, ni vigumu sana yeye kuwa ndiye
aliyeandika wakati kifo chake kimeandikwa katika 1Samweli 25. Ye yote aliyeandika vitabu hivi anaweza kuwa
alitumia kitabu cha Yashari, ambacho kimetajwa katika 2Samweli 18 kama chanzo cha habari hizi. Uandishi wa
Samweli, nabii Nathani na Gadi, “Daudi mwana wa Yese alitawala juu ya Israeli miaka arobaini: Alitawala huko
Hebroni miaka saba na miaka thelatini na mitatu akatawala huko Yerusalemu” (1Mambo ya Nyakati 29:29.).
Hawa ndio ambao wameeleza matendo yote ya Mfalme Daudi tangu mwanzo hadi mwisho.
Wahusika Wakuu
Eli, Elikana, Hana, Samweli, Sauli, Yonathani, Daudi.
Mahali
Kitabu kinaanzia wakati walipokuwa wanaongozwa na waamuzi na kuelezea Israeli kuondoka katika utawala
wa Mungu na kuingia katika utawala wa wanadamu kwa kuwa na mfalme.
Tarehe
1204 – 1035 K.K.
Mgawanyo
Eli kuhani na mwamuzi (1:1-4:22)
Samweli kiongozi wa Israeli (5:1-8:22)
Sauli mfalme wa kwanza wa Israeli (9:1-15:35)
Kifo cha Sauli (31:1-13).
1
1SAMWELI
Kuzaliwa Kwa Samweli
Kulikuwepo na mtu mmoja kutoka Rama,
Msufi kutoka nchi ya vilima vya Efraimu,
ambaye jina lake aliitwa Elikana mwana wa
Yerohamu, mwana wa Elihu mwana wa Tohu,
mwana wa Sufu, Mwefraimu. 2 Alikuwa na wake
wawili, mmoja aliitwa Hana na mwingine Penina.
Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa
na mtoto.
3 Kila mwaka mtu huyu alikwea kutoka mji
wake ili kuabudu na kutoa dhabihu kwa BWANA
Mwenye Nguvu huko Shilo, ambapo Hofni na
Finehasi, wana wawili wa Eli, walikuwa
makuhani wa BWANA. 4 Kila mara ilipofika siku
ya Elikana kutoa dhabihu, aliwapa mafungu
Penina mkewe na wanawe wote pamoja na binti
zake. 5 Lakini alimpa Hana fungu mara dufu kwa
sababu alimpenda, ingawa BWANA alikuwa
amemfunga tumbo. 6 Kwa sababu BWANA
alikuwa amemfunga tumbo, mke mwenzake
alikuwa anamchokoza ili kumwudhi. 7 Hili
liliendelea mwaka baada ya mwaka. Kila mara
Hana alipokwenda katika nyumba ya BWANA,
mke mwenzake alikuwa akimkasirisha mpaka
analia na kushindwa kula. 8 Elikana mumewe
akawa anamwambia, “Hana, kwa nini unalia?
Kwa nini huli? Kwa nini kuvunjika moyo? Je,
mimi si bora zaidi kwako kuliko watoto kumi?’’
9 Siku moja walipokuwa wamemaliza kula na
kunywa huko Shilo, Hana alisimama. Wakati huo
kuhani Eli alikuwa ameketi kwenye kiti pembeni
mwa mwimo wa mlango wa hekalu la BWANA.
10 Kwa uchungu wa rohoni Hana alilia sana na
akamwomba BWANA. 11 Naye akaweka nadhiri,
akisema, “Ee BWANA Mwenye Nguvu, laiti
ungeangalia huzuni kuu ya mtumishi wako na
kunikumbuka mimi, wala
usimsahau mtumishi wako nawe ukampa
mwana, basi huyo mwana nitamtoa kwa
BWANA kwa siku zote za maisha yake, wala
wembe hautapita kichwani mwake.
12 Alipokuwa anaendelea kumwomba
BWANA, Eli alichunguza kinywa chake. 13 Hana
alikuwa akiomba moyoni mwake midomo yake
ikiwa inachezacheza lakini sauti haikusikika. Eli
akafikiri alikuwa amelewa 14 naye akamwambia,
“Utaendelea kulewa mpaka lini? Achilia mbali
mvinyo wako.’’
15 Hana akajibu, “Si hivyo bwana wangu,
mimi ni mwanamke mwenye huzuni kubwa. Mimi
sijanywa mvinyo wala kileo, nilikuwa
ninaumimina moyo wangu kwa BWANA.
16 Usimdhanie mtumishi wako kuwa mwanamke
mwovu, nimekuwa nikiomba hapa katika wingi
wa uchungu mkuu na huzuni.’’
17 Eli akamjibu, “Nenda kwa amani, naye
Mungu
1
wa
Israeli
na
akujalie
kile
ulichomwomba.’’
18 Hana akasema, “Mtumishi wako na apate
kibali machoni pako.’’ Kisha akaondoka zake na
kula chakula wala uso wake haukuwa na huzuni
tena.
19 Kesho yake asubuhi na mapema waliamka
wakaabudu mbele za BWANA na kisha
wakarudi nyumbani kwao huko Rama. Elikana
akakutana kimwili na mkewe Hana, naye
BWANA akamkumbuka. 20 Hivyo wakati
ulipotimia, Hana akapata mimba na akamzaa
mwana. Hana akamwita jina lake Samweli,
akasema,
“Kwa
kuwa
nilimwomba
kwa
BWANA.’’
Hana Anamweka Samweli Wakfu.
21 Wakati huyo mtu Elikana alipopanda
pamoja na jamaa yake yote kutoa dhabihu ya
mwaka kwa BWANA na kutimiza nadhiri yake,
22 Hana hakwenda. Alimwambia mume wake,
“Baada ya mtoto kuachishwa kunyonya,
nitamchukua na kumpeleka mbele za BWANA,
naye ataishi huko wakati wote.’’
23 Elikana mumewe akamwambia, “Fanya lile
unaloona ni bora zaidi kwako. Ukae hapa mpaka
utakapomwachisha kunyonya, BWANA na
akujalie kutimiza nadhiri yako.’’ Hivyo huyo
mwanamke akakaa nyumbani na kunyonyesha
mwanawe mpaka alipomwachisha kunyonya.
24 Baada ya mtoto kuachishwa kunyonya,
Hana akamchukua huyo mtoto, akiwa mdogo
hivyo hivyo pamoja na fahali wa miaka mitatu,
ef a a ya unga na kiriba cha divai, naye akamleta
mtoto kwenye nyumba ya BWANA huko Shilo.
25 Wakati walipokwisha kumchinja yule fahali;
wakamleta mtoto kwa Eli, 26 Hana akamwambia
Eli, “Hakika kama uishivyo, bwana wangu, mimi
ndiye yule mama ambaye alisimama hapa
karibu nawe akiomba kwa BWANA. 27 Niliomba
mtoto huyu, naye BWANA amenijalia kile
nilichomwomba. 28 Hivyo sasa ninamtoa kwa
BWANA. Kwa maana maisha yake yote atakuwa
ametolewa kwa BWANA.’’ Naye akamwabudu
BWANA huko.
24 “Efa moja” ni kipimo cha kilo 22
2
952102415.004.png
 
1SAMWELI
Maombi Ya Hana
Kisha Hana akaomba na kusema:
“Moyo wangu wamshangilia BWANA,
katika BWANA pembe yangu
imeinuliwa juu.
Kinywa changu chajisifu juu ya adui zangu,
kabisa.
Atapiga radi dhidi yao kutoka mbinguni,
2
BWANA ataihukumu miisho ya dunia.
“Atampa nguvu mfalme wake
na kuitukuza pembe ya mpakwa mafut a b
kwa kuwa naufurahia wokovu wako.
wake.’’
2 “Hakuna ye yote aliye mtakatifu kama BWANA,
hakuna mwingine zaidi yako,
hakuna Mwamba kama Mungu wetu.
3 “Msiendelee kusema kwa kiburi hivyo
wala msiache vinywa vyenu kunena kwa
kiburi,
kwa kuwa BWANA ndiye Mungu ajuaye,
na kwa Yeye matendo hupimwa.
4 “Pinde za mashujaa zimevunjika,
lakini wale wanaojikwaa wamevikwa nguvu.
5 Wale waliokuwa na chakula tele wamejikodisha
wenyewe ili kupata chakula,
lakini wale waliokuwa na njaa hawana njaa
tena.
Mwanamke yule aliyekuwa tasa amezaa watoto
11 Kisha Elkana akaenda nyumbani Rama,
lakini mtoto akahudumu mbele za BWANA chini
ya kuhani Eli.
Wana Waovu Wa Eli
12 Wana wa Eli walikuwa watu wabaya
kabisa, hawakumheshimu BWANA. 13 Basi
ilikuwa desturi ya makuhani pamoja na watu
kwamba kila mara ye yote anapotoa dhabihu na
huku nyama ikiwa inachemshwa, mtumishi wa
kuhani angalikuja na uma wenye meno matatu
mkononi mwake. 14 Angeutumbukiza huo uma
kwenye sufuria au birika au sufuria kubwa au
chungu, naye kuhani angalijichukulia mwenyewe
cho chote ambacho uma ungelikileta. Hivi ndivyo
walivyowatendea Waisraeli wote waliokuja Shilo.
15 Lakini hata kabla mafuta ya mnyama
hayajachomwa, mtumishi wa kuhani angalikuja
na kusema kwa mtu ambaye alikuwa akitoa
dhabihu, “Mpe kuhani nyama akaoke, kwani
hatapokea nyama iliyochemshwa kutoka kwako,
ila iliyo mbichi tu.’’
16 Kama mtu akimwambia, “Mafuta ya
mnyama na yachomwe kwanza, kisha ndipo
uchukue cho chote unachotaka,” mtumishi
angalijibu, “Hapana, nipe sasa, kama huwezi
nitaichukua kwa nguvu.’’
17 Hii Dhambi ya hawa vijana ilikuwa kubwa
sana machoni pa BWANA, kwa kuwa
waliitendea dhabihu ya BWANA kwa dharau.
18 Lakini Samweli alikuwa akihudumu mbele
za BWANA, kijana akivaa kisibau cha kitani.
19 Kila mwaka mama yake alimshonea joho dogo
na kumchukulia wakati alipokwea pamoja na
mumewe kutoa dhabihu ya mwaka. 20 Eli alikuwa
akiwabariki Elkana na mkewe, akisema,
“BWANA na akupe watoto kwa mwanamke huyu
ili kuchukua nafasi ya yule aliyekuwa
amemwomba na akamtoa kwa BWANA. Kisha
wakawa wanakwenda nyumbani. 21 BWANA
akawa mwenye neema kwa Hana, naye akapata
mimba akazaa wana watatu na binti wawili.
saba,
lakini yule ambaye alikuwa na wana wengi
amedhoofika.
6 “BWANA huua na huleta uhai,
hushusha chini mpaka kaburini a na kufufua.
7 BWANA humfanya mtu maskini naye
hutajirisha,
hushusha na hukweza.
8 Humwinua maskini kutoka mavumbini
na humwinua mhitaji kutoka lundo la majivu;
huwaketisha pamoja na wakuu
na kuwafanya warithi kiti cha enzi cha
heshima.
“Kwa kuwa misingi ya dunia ni ya BWANA,
juu yake ameuweka ulimwengu.
9 Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake,
lakini waovu watanyamazishwa kwenye
i .
“Si kwa nguvu mtu hushinda,
10 wale wampingao BWANA wataharibiwa
10 “Mpakwa mafuta” hapa maana yake “Masihi” yaani,
“Aliyetiwa mafuta”
a 6 “Kaburini” hapa ina maana “Kuzimu”, yaani, kwa Kiebrania
“Sheol”
3
952102415.005.png 952102415.006.png 952102415.001.png
1SAMWELI
Wakati huo, kijana Samweli akaendelea kukua
mbele za BWANA.
22 Basi Eli, ambaye alikuwa mzee sana,
alisikia kuhusu kila kitu ambacho wanawe
walikuwa wakiwafanyia Israeli wote na jinsi
walivyokutana kimwili na wanawake
waliohudumu kwenye ingilio la Hema la
Mkutano. 23 Hivyo akawaambia, “Kwa nini
mmefanya mambo kama haya? Nimesikia
kutoka kwa watu wote juu ya haya matendo
yenu maovu. 24 Sivyo, wanangu, hii si habari
nzuri ambayo ninasikia ikienea miongoni mwa
watu wa BWANA. 25 Kama mtu akifanya dhambi
dhidi ya mtu mwenzake, mtu mwingine aweza
kumwombea kwa Mungu, lakini kama mtu
akimfanyia Mungu dhambi, ni nani
atakayemwombea? Hata hivyo wanawe
hawakusikia maonyo ya baba yao, kwa sababu
BWANA alitaka kuwaua.
26 Naye kijana Samweli akaendelea kukua
katika
kuwa mzee. 33 Kila mmoja wenu ambaye
sitamkatilia mbali kutoka madhabahuni pangu
atabakizwa tu kupofusha macho yenu kwa
machozi na kuihuzunisha mioyo yenu, nao
wazao wenu wote watakufa watakapokuwa
wamefikia umri wa kustawi.
34 Kile kitakachotokea kwa wanao wawili,
Hofni na Finehasi, kitakuwa ishara kwako. Wote
wawili watakufa katika siku moja. 35 Mimi
mwenyewe nitajiinulia kuhani mwaminifu,
ambaye atafanya sawasawa na kile kilichoko
moyoni mwangu na akilini mwangu. Nitaifanya
nyumba yake kuwa imara, naye atahudumu
mbele ya mpakwa mafuta wangu daima. 36 Kisha
kila mmoja aliyeachwa katika mbari yenu atakuja
na kusujudu mbele yake kwa ajili ya kipande cha
fedha na ganda la mkate akisema, “Niteue
katika baadhi ya ofisi ya ukuhani ili niweze
kupata chakula.’’
kimo
akimpendeza
BWANA
na
BW
ANA Amwita Samweli
3
wanadamu.
Kijana Samweli alihudumu mbele za
BWANA chini ya Eli. Katika siku zile neno
la Mungu lilikuwa adimu, hapakuwepo na maono
mengi.
Unabii Dhidi Ya Nyumba Ya Eli
27 Basi mtu wa Mungu akaja kwa Eli na
kumwambia, “Hivi ndivyo asemavyo BWANA :
‘Je, sikujifunua wazi wazi kwa nyumba ya baba
yako wakati walipokuwa huko Misri chini ya
Farao? 28 Nilimchagua baba yako kati ya
makabila yote ya Israeli kuwa kuhani wangu,
kukwea kwenye madhabahu yangu, kufukiza
uvumba na kuvaa kisibau mbele yangu. Pia
niliwapa nyumba ya baba yako sadaka zote
zilizotolewa kwa moto na Waisraeli. 29 Kwa nini
unadharau dhabihu zangu na sadaka zile
nilizoziamuru kwa ajili ya makao yangu? Kwa
nini unawaheshimu wanao kuliko mimi kwa
kujinenepesha wenyewe kwa kula zile sehemu
zilizo bora za kila sadaka zinazotolewa na watu
wangu wa Israeli?
30 “Kwa hiyo, BWANA, Mungu wa Israeli
asema: “Niliahidi kuwa nyumba yako na nyumba
ya baba yako wangehudumu mbele zangu
milele”. Lakini sasa BWANA anasema: Jambo
hili na liwe mbali nami! Wale wanaoniheshimu
nitawaheshimu, wale wanaonidharau mimi
watadharauliwa. 31 Wakati unakuja
nitakapozipunguza nguvu zenu na nguvu ya
nyumba ya baba yenu, ili pasiwepo mtu katika
mbari yenu atakayeishi kuuona uzee 32 nanyi
mtaona huzuni katika makao yangu. Ingawa
Israeli watafanyiwa mema, katika mbari yenu
kamwe hapatakuwepo mtu atakayeishi hadi
2 Usiku mmoja Eli, ambaye macho yake
yalikuwa yamefifia sana kiasi kwamba aliona
kwa shida sana, alikuwa amelala mahali pake pa
kawaida. 3 Taa ya Mungu ilikuwa haijazimika
bado na Samweli alikuwa amelala hekaluni a
mwa BWANA, ambapo sanduku la Mungu
lilikuwako. 4 Kisha BWANA akamwita Samweli.
Samweli akajibu, “Mimi hapa.’’ 5 Naye
akakimbia kwa Eli na kumwambia, “Mimi hapa,
kwa kuwa umeniita.’’
Lakini Eli akasema, “Sikukuita, rudi ukalale.’’
Hivyo akaenda kulala.
6 BWANA akaita tena, “Samweli!’’ Naye
Samweli akaamka, kwenda kwa Eli na kusema,
“Mimi hapa, kwa kuwa umeniita’’
Eli akasema, “Mwanangu, sikukuita, rudi
ukalale.’’
7 Wakati huu Samweli alikuwa bado
hajamjua BWANA. Neno la BWANA lilikuwa
bado halijafunuliwa kwake.
8 BWANA akamwita Samweli mara ya tatu,
naye Samweli akaamka kwenda kwa Eli na
kusema, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.’’
Ndipo Eli akatambua kuwa BWANA alikuwa
akimwita kijana. 9 Hivyo Eli akamwambia
Samweli, “Nenda ukalale, na kama akikuita,
sema, ‘Nena BWANA, kwa kuwa mtumishi wako
a 3 “Hekalu” hapa ina maana “Maskani ya BWANA ”
4
952102415.002.png
 
1SAMWELI
anasikiliza.’’ Hivyo Samweli akaenda na kulala
mahali pake.
10 BWANA akaja akasimama hapo, akiita
kama mara zile nyingine, “Samweli! Samweli!”
Kisha Samweli akasema, “Nena, kwa kuwa
mtumishi wako anasikiliza.’’
11 Naye BWANA akamwambia Samweli:
“Tazama, nipo karibu kufanya kitu katika Israeli
ambacho kitafanya masikio ya kila mmoja
atakayesikia yawashe. 12 Wakati huo nitatimiza
dhidi ya Eli kila kitu nilichonena dhidi ya jamaa
yake, kuanzia mwanzo mpaka mwisho. 13 Kwa
kuwa nilimwambia kwamba ningehukumu jamaa
yake milele kwa sababu ya dhambi aliyoijua,
wanawe kumkufuru Mungu, naye akashindwa
kuwazuia. 14 Kwa hiyo, nikaapa kuhusu nyumba
ya Eli, “Hatia ya nyumba ya Eli kamwe
haitaweza kufidiwa kwa dhabihu au sadaka.’’
15 Samweli akalala mpaka asubuhi, kisha
akafungua milango ya nyumba ya BWANA.
Aliogopa kumwambia Eli yale maono, 16 lakini Eli
akamwita
agano la BWANA kutoka Shilo, ili kwamba lipate
kwenda pamoja nasi na kutuokoa kutoka mkono
wa adui zetu.’’
4 Hivyo wakatumwa watu kwenda Shilo, nao
wakalichukua sanduku la agano la BWANA
Mwenye Nguvu, aliyekaa kwenye kiti chake cha
enzi kati ya makerubi. Nao wale wana wawili wa
Eli, Hofni na Finehasi, walikuwako huko pamoja
na sanduku la agano la Mungu.
5 Wakati sanduku la agano la BWANA
lilipokuja kambini, Waisraeli wote wakapiga
kelele kwa sauti kuu hata ardhi ikatikisika.
6 Wafilisti waliposikia makelele wakauliza, “Ni nini
makelele
haya
yote
katika
kambi
ya
Waebrania?’’
Walipofahamu kuwa sanduku la BWANA
limekuja kambini, 7 Wafilisti wakaogopa
wakasema, “Mungu amekuja kambini, ole wetu.’’
Halijatokea jambo kama hili tangu hapo. 8 Ole
wetu! Ni nani atakayetuokoa kutoka mikononi
mwa miungu hii yenye nguvu? Ni miungu ile
iliyowapiga Wamisri kwa mapigo ya aina zote
huko jangwani. 9 Tuweni hodari, enyi Wafilisti!
Tuweni wanaume, la sivyo mtakuwa watumwa
wa Waebrania, kama wao walivyokuwa kwenu.
Iweni wanaume, mpigane!’’
10 Basi Wafilisti wakapigana, nao Waisraeli
wakashindwa na kila mtu akakimbilia hemani
mwake. Mauaji yalikuwa makubwa sana, Israeli
wakapoteza askari 30,000 waendao kwa miguu.
11 Sanduku la Mungu likatekwa, na hao wana
wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, wakauawa.
na
kumwambia,
“Samweli
mwanangu.’’
Samweli akamjibu, “Mimi hapa.’’
17 Eli akamwuliza, “Ni nini alichokuambia?
Usinifiche. BWANA na ashughulike nawe, tena
kwa ukali, kama utanificha cho chote
alichokuambia.’’ 18 Kwa hiyo Samweli
akamwambia kila kitu, bila kumficha cho chote.
Ndipo Eli akasema, “Yeye ni BWANA na afanye
lile lililo jema machoni pake!’’
19 BWANA alikuwa pamoja na Samweli
alipokuwa akikua na hakuacha hata moja ya
maneno yake lianguke chini. 20 Nao Israeli wote
kuanzia Dani hadi Beer-Sheba wakatambua
kuwa Samweli amethibitishwa kuwa nabii wa
BWANA. 21 BWANA akaendelea kutokea huko
Shilo na huko kujidhihirisha kwa Samweli kwa
njia ya neno lake.
Kifo Cha Eli
12 Siku ile ile mtu mmoja wa kabila la
Benyamini akakimbia kutoka kwenye uwanja wa
vita na kwenda Shilo, nguo zake zikiwa
zimeraruka na akiwa na mavumbi kichwani
mwake. 13 Alipofika, Eli alikuwa ameketi juu ya
kiti chake kando ya barabara akiangalia, kwa
sababu moyo wake ulikuwa na hofu kwa ajili ya
sanduku la Mungu. Mtu yule alipoingia mjini na
kueleza ni nini kilichokuwa kimetokea, mji wote
ukalia.
14 Eli akasikia kelele za kilio naye akauliza,
“Ni nini maana ya makelele haya?
Yule mtu akafanya haraka kwenda kwa Eli,
15 wakati huu Eli alikuwa na miaka tisini na
minane nayo macho yake yalikuwa yamepofuka
na hakuweza kuona. 16 Akamwambia Eli, “Mimi
nimetoka vitani sasa hivi, nimekimbia kutoka
huko leo hii.’’
Waf
ilisti Wateka Sanduku La Mungu
4
Nalo neno la Samweli likaja kwa Israeli
yote. Basi Waisraeli walitoka kwenda
kupigana dhidi ya Wafilisti. Waisraeli wakapiga
kambi huko Ebenezeri, nao Wafilisti wakapiga
kambi huko Afeki. 2 Wafilisti wakapanga safu za
majeshi yao kupambana na Israeli, wakati vita
vilipoenea, Israeli wakashindwa na Wafilisti,
ambao waliwaua askari wa Israeli wapatao
4,000 kwenye uwanja wa vita. 3 Wakati Askari
waliporudi kambini, wazee wa Israeli
wakawauliza, “Kwa nini BWANA ameruhusu leo
tushindwe mbele ya Wafilisti? Tulete sanduku la
Eli akamwuliza, “Je, mwanangu, ni nini
5
952102415.003.png
 
Zgłoś jeśli naruszono regulamin