RUT_Kiswahili_1068.pdf

(53 KB) Pobierz
RUTHI
Utangulizi
Kitabu hiki kinachukua jina la mhusika wake mkuu, yaani, Yoshua, mwana wa Nuni, ambaye anatoka
kwenye kabila la Efraimu (Hes.13:8). Yoshua maana yake Yehova (BWANA) ni wokovu. Yoshua alichaguliwa na
Mungu kuwa kiongozi muda mfupi kabla ya kifo cha Mose (Kum.31).
Maandalizi kwa ajili ya huduma yake yanajumuisha: Kiongozi wa jeshi la Israeli kupigana na Waamaleki
(Kut..17:8-16) ; msaidizi wa Mose( Kut..33:11) ; mmoja wa wale wapelelezi kumi na wawili waliokwenda
kupeleleza Kanaani (Hes.13-14); kuchaguliwa kwake kuingia mahali pa Mose kwa sababu ya kujionyesha kwa
kipekee kwa huduma yake( Hes.27:18 - 23; 32:13; Kum.1:38; 31:7- 8)
Kitabu cha Yoshua ni habari juu ya Waisraeli wakiongozwa na Yoshua. Yoshua ambaye bila shaka
kufanikiwa kwake kunasababishwa na hali yake kumwelekea Munguna ufunuo wa Mose, mara anwafanya
Waisraeli watambue uhusiano wao na Mungu kwa kuadhimisha Pasaka(5:10) na kanuni ya tohara(5:3) na kwa
kusimamisha kumbukumbu ya jiwe (4:3) baada ya kuvuka Mto Yordani. Waisraeli walivuka Mto Yordani
kimwujiza. Kutokana na vile mji wa Yeriko ulivyotekwa kwa mwujiza(5:13 -627), ungeweza ukawa ndio msingi
wao wa imani katika Mungu kwamba sehemu iliyosalia ya Kanaani pia ingekaliwa na wao. Kule kutekwa kwa mji
wa Ai, kushindwa kwa umoja wa Waamori upande wa kusini, kule kuanguka kwa Hazori, iliyokuwa ngome ya
Wakanaani upande wa kaskazini, kuliwapa Waisraeli kumiliki sehemu muhimu za nchi ya Ahadi, yaani, Kanaani.
Ingawa makabila mawili na nusu, yaani, kabila la Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase tayari
walikwisha kumiliki eneo la mashariki mwa Mto Yordani chini ya uongozi wa Mose, makabila mengine yaliyosalia
yalipata sehemu zao chini ya uongozi wa Yoshua. Kabila la Lawi halikupewa mgao wa urithi katika nchi, bali wao
walipewa miji arobaini na minane kuwa miliki yao katika nchi nzima ili waweze kutoa huduma yao ya kiroho kwa
sababu wao walipewa ukuhani.
Kabla Yoshua hajafa aliwakumbusha watu juu ya agano la Mungu na ahadi Zake kwao, akawaonya kuhusu
kuabudu sanamu.Yeye aliweka wazi upya agano kati ya Mungu na Israeli, akiwaonya Waisraeli kudumisha ile
hali ya kujitoa kwa Mungu na kumpenda kwa moyo wote.Aliwaelekeza watu waendelee kumpenda, kumtii na
kumtumikia Mungu. Alizungumza hadharani jinsi ambavyo yeye binafsi alikuwa tayari kumtumikia Mungu
aliposema, “….Chagueni hivi leo mtakayemtumikia, lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA..” (24:15)
Wazo Kuu
Kuvuka Mto Yordani kwa mwujiza, kuingia, kutekwa na kugawanywa kwa Nchi ya Ahadi – Kanaani.
Miongoni mwa wanaume 603,550 wenye umri wa miaka kuanzia ishirini wawezao kwenda vitani waliotoka Misri,
ni Yoshua na Kalebu peke yao ndio walioingia Nchi ya Ahadi, yaani, Kanaani.
Mwandishi
Mwandishi kitabu hiki ni Yoshua,kiongozi wa Israeli baada ya Mose, isipokuwa sehemu ya mwisho ambayo
mwandishi wake hajulikani, lakini mapokeo ya Kiyahudi yanasema kwamba (24:29-32) iliongezwa na Eleazari na
( mst..33) uliandikwa na kuhani Finehasi, shahidi ambaye alishuhudia kwa macho yake mambo yaliyoandikwa
humu.
Mahali
Kanaani, ambayo ndiyo iliyokuwa Nchi ya Ahadi. Kwa sasa ndiyo nchi ya Israeli.
Tarehe
1646 – 1616 K.K. kwani matukio yaliyomo ni yale yaliyotukia wakati huo.
Wahusika Wakuu
Yoshua, Rahabu, Akani, Finehasi, Eleazari.
Mgawanyo
Maandalizi ya kuiteka Kanaani. (1:1-5:15)
Kuishinda Kanaani. (6:1-12:24)
Mgawanyo wa nchi kwa makabila. (13:1-21:45)
Kuagana na Yoshua na kifo chake. (22:1-24:33)
1
RUTHI
Naomi na Ruthi
Wakati Waamuzi walipotawala Israeli,
kulikuwa na njaa katika nchi, akaondoka
mtu mmoja kutoka nchi ya Bethlehemu ya Yuda
pamoja na mke wake na wanae wawili, akaenda
kuishi katika nchi ya Moabu. 2 Mtu huyu aliitwa
Elimeleki, mkewe aliitwa Naomi, na hao wanawe
wawili waliitwa Maloni na Kilioni. Walikuwa
Waefrathi kutoka Bethlehemu ya Yuda.
Wakaenda katika nchi ya Moabu wakaishi huko.
3 Elimeleki mumewe Naomi akafa, Naomi
akabaki na wanawe wawili. 4 Nao wakaoa
wanawake wa Kimoabu, jina la mmoja aliitwa
Orpa na wa pili aliitwa Ruthi. Baada ya miaka
kumi, 5 Maloni na Kilioni pia wakafa, basi Naomi
akabaki hana mume wala wanawe wawili.
6 Aliposikia huko Moabu kwamba BWANA
amewasaidia watu wake kwa kuwapa chakula,
Naomi na wakweze wakajiaandaa kurudi
nyumbani. 7 Yeye na wakweze wawili,
wakaondoka pale walipokuwa wakiishi na
kushika njia kurudi nchi ya Yuda.
8 Ndipo Naomi akawaambia wale wakwe
zake wawili, “Rudini, kila mmoja wenu nyumbani
kwa mama yake. BWANA na awatendee fadhili
kama mlivyowatendea hao waliofariki pamoja na
mimi. 9 BWANA na amjalie kila mmoja wenu
maisha mema nyumbani kwa mume mwingine.”
Kisha akawabusu, nao wakalia kwa sauti
kubwa 10 wakamwambia, “Tutarudi pamoja na
wewe nyumbani kwa watu wako.”
11 Lakini Naomi akasema, “Rudini nyumbani,
binti zangu. Kwa nini mnifuate? Mimi nitaweza
tena kuwa na wana wengine, ambao wataweza
kuwaoa ninyi? 12 Rudini nyumbani binti zangu,
mimi ni mzee kiasi kwamba siwezi kumpata
mume mwingine. Hata kama ningefikiria kuwa
bado kuna tumaini kwangu, hata kama
ningekuwa na mume usiku huu na kuwazaa
wana, 13 je, mngesubiri mpaka wakue?
Mngebakia bila kuolewa mkiwasubiri? La,
hasha, binti zangu. Nimepata uchungu kuliko
ninyi, kwa sababu mkono wa BWANA umekuwa
kinyume nami!”
14 Kisha wakalia tena kwa sauti. Orpa
akambusu mama mkwe wake akaenda zake,
lakini Ruthi akaambatana naye.
15 Naomi akamwambia, “Tazama, mwenzako
anarejea kwa watu wake na kwa miungu yake.
Rudi pamoja naye.”
16 Lakini Ruthi akajibu, “Usinisihi nikuache au
niache kukufuata. Utakakokwenda nami
nitakwenda, na wewe utakapoishi nitaishi. Watu
wako watakuwa watu wangu na Mungu wako
atakuwa Mungu wangu. 17 Pale utakapofia nami
1
nitafia hapo na papo hapo nitazikwa.BWANA na
aniadhibu vikali, kama kitu kingine cho chote
kitanitenga nawe isipokuwa kifo.” 18 Naomi
alipotambua kwamba Ruthi amenuia kufuatana
naye, hakuendelea kumsihi tena.
19 Kwa hiyo hao wanawake wawili
wakaondoka wakafika Bethlehemu. Walipofika
Bethlehemu, mji mzima ulitaharuki, wanawake
wakashangaa wakasema, “Huyu aweza kuwa ni
Naomi?”
20 Akawaambia, “Msiniite tena Naomi a , niiteni
Mar a b , kwa sababu Mwenyezi Mungu
amenitendea mambo machungu sana. 21 Mimi
niliondoka hali nimejaa, lakini BWANA
amenirudisha mtupu. Kwa nini kuniita Naomi?
BWANA amenitendea mambo machungu,
Mwenyezi Mungu ameniletea msiba.”
22 Kwa hiyo Naomi alirudi pamoja na Ruthi
Mmoabi, mkwe wake, nao wakafika Bethlehemu
mwanzoni mwa kuvuna shayiri.
Ruthi Akutana na Boazi
Basi Naomi alikuwa na jamaa wa upande
wa mume wake, kutoka katika ukoo wa
Elimeleki, jina lake aliitwa Boazi.
2 Ruthi Mmoabi akamwambia Naomi,
“Nitakwenda mashambani nikaokote mabaki ya
nafaka nyuma ya yule nitakayepata kibali
machoni pake.”
Naomi akamwambia, “Nenda, binti yangu.”
3 Basi akaenda akaokota mabaki ya nafaka
nyuma ya wavunaji. Ikatokea kwamba, alijikuta
anafanya kazi kwenye shamba lililokuwa mali ya
Boazi, ambaye alitoka kwenye ukoo wa
Elimeleki.
4 Papo hapo Boazi akarudi kutoka
Bethlehemu akawasalimu wavunaji akasema,
“BWANA awe nanyi!” Nao wakamjibu,
“BWANA akubariki.”
5 Boazi akamwuliza msimamizi wa wavunaji,
“Je, huyo mwanamwali ni wa nani?”
6 Msimamizi akamjibu, “Yeye ni yule Mmoabi
aliyerudi kutoka nchi ya Moabu pamoja na
Naomi. 7 Yeye aliomba, ‘Tafadhali niruhusu
niokote na kukusanya miongoni mwa minganda
nyuma ya wavunaji.’ Naye ameshinda shambani
tangu asubuhi pasipo kupumzika, isipokuwa kwa
muda mfupi kivulini.”
2
20 Naomi: maana yake ni “wa kupendeza’’
20 Mara: maana yake ni “Chungu.”
2
952102457.003.png
 
RUTHI
8 Kisha Boazi akamwambia Ruthi, “Binti
yangu, nisikilize, usiende kuokota mabaki ya
mavuno katika shamba lingine na usiondoke
hapa. Kaa hapa na hawa watumishi wangu wa
kike. 9 Angalia shamba wanamovuna, ufuate
nyuma yao. Nimewaamuru hao wanaume
wasikuguse. Wakati wo wote ukiona kiu, nenda
kwenye mitungi ukanywe maji waliyoyateka hao
wanaume.’’
fadhili zake kwa walio hai na kwa hao
waliokufa.” Pia akamwambia, “Huyo mtu ni
mmoja wa jamaa yetu wa karibu anayestahili
kukomboa.’’
21 Kisha Ruthi Mmoabi akasema, “Hata
aliniambia, ‘Kaa pamoja na watumishi wangu
mpaka watakapomaliza kuvuna nafaka yangu
yote.’”
22 Kisha Naomi akamwambia Ruthi mkwewe,
“Binti yangu, itakuwa vema wewe ufuatane na
wasichana wake, kwa sababu katika shamba la
mtu mwingine wanaweza kukudhuru.”
23 Kwa hivyo Ruthi akafuatana na watumishi
wasichana wa Boazi kuokota mpaka mwisho wa
mavuno ya shayiri na ya ngano. Naye aliishi na
mama mkwe wake.
10 Kwa ajili ya hili akasujudu mpaka nchi,
akamwambia, “Ni kwa nini nimepata kibali
machoni pako hata ukanijali mimi, mgeni?”
11 Boazi akamjibu, “Nimeambiwa yote
uliyomtendea mama mkwe wako tangu mume
wake alipofariki, na jinsi ulivyomwacha baba
yako na mama yako na nchi yako ulimozaliwa,
ukaja kuishi na watu ambao hukuwafahamu. 12
na akulipe kwa yale uliyoyatenda. Ubarikiwe kwa
wingi na BWANA wa Israeli, ambaye
umekimbilia mbawani mwake.”
13 Kisha Ruthi akasema, “Naomba niendelee
kupata kibali machoni pako bwana wangu. Kwa
maana umenifariji na umezungumza kwa
ukarimu na mjakazi wako, hata ingawa mimi si
bora kama mmoja wa watumishi wako wa kike.”
14 Wakati wa chakula Boazi akamwambia
Ruthi, “Karibia hapa. Kula mkate na uchovye
ndani ya divai.”
Alipoketi pamoja na wavunaji, akampa
nafaka zilizookwa. Akala kiasi alichotaka na
kusaza. 15 Alipoinuka ili kuokota mabaki ya
nafaka, Boazi akawaagiza watu wake, “Hata
kama atakusanya kati ya miganda msimzuie.
16 Badala yake toeni masuke katika miganda
mwacheni ayaokote na msimkemee.’’
17 Basi Ruthi akaokota masazo kondeni hata
jioni. Akatwanga ile shayiri aliyokusanya, ikajaa
efa moja a . 18 Akaibeba na kuelekea mjini, mama
mkwe wake akaona jinsi alivyoweza kuokota
nafaka nyingi. Pia Ruthi akachukua kile
alichobakiza baada ya kula na kushiba, akampa.
19 Basi mkwewe akamwuliza, “Je, umeokota
wapi leo? Umefanya kazi wapi? Abarikiwe mtu
yule aliyekujali.”
Ndipo Ruthi akamwambia mama mkwe
wake juu ya yule ambaye yeye alikuwa
amefanyia kazi katika shamba lake. Akasema,
“Yule mtu niliyefanyia kazi kwake leo, anaitwa
Boazi.”
20 Naye Naomi akamwambia mkwewe,
“BWANA ambariki! Hakuacha kuonyesha
Ruthi na Boazi Kwenye Sakafu ya Kupuria
Kisha Naomi akamwambia mkwewe, “Binti
yangu, je, nisingelikutafutia pumziko
ambako utatunzika vema? 2 Je, Boazi, ambaye
umekuwa pamoja na watumishi wake
wasichana, si jamaa yetu wa karibu? Usiku wa
leo atakuwa anapepeta ngano kwenye sakafu ya
kupuria. 3 Basi oga na ukajipake marashi, ujivalie
nguo zako nzuri. Kisha uende kwenye sakafu ya
kupuria, lakini angalia asijue kwamba upo pale
mpaka atakapomaliza kula na kunywa.
4 Atakapokwenda kulala, angalia mahali
atakapolala. Kisha uende ufunue miguu yake,
ulale. Naye atakuambia utakalofanya.’’
3
5 Ruthi akajibu, “Lo lote usemalo nitatenda.”
6 Basi akashuka mpaka kwenye sakafu ya
kupuria, akafanya kila kitu mama mkwe wake
alichomwambia kufanya.
7 Wakati Boazi alipomaliza kula na kunywa,
naye alikuwa amejawa na furaha, alikwenda
kulala mwisho wa lundo la nafaka. Ruthi
akakaribia kimya kimya, akafunua miguu yake
akalala. 8 Usiku wa manane kitu kilimshtua
Boazi, akajigeuza, akagundua yupo mwanamke
amelala miguuni pake.
9 Akauliza, “Wewe ni nani?’’
Akajibu, “Ni mimi Ruthi mjakazi wako.
Uitande nguo yako juu yangu kwa sababu wewe
ndiwe jamaa wa karibu wa kukomboa.
10 Akamwambia, “Binti yangu, ubarikiwe na
BWANA. Wema huu wa sasa ni mkuu kushinda
hata ule ulioonyesha mwanzoni. Hukuwakimbilia
vijana, wakiwa matajiri au maskini. 11 Sasa, binti
yangu, usiogope. Nitakufanyia yote uliyoomba.
Kwa maana mji wote wa watu wangu wanakujua
ya kwamba
a 17 Efa moja ni sawa na kilo 20
3
952102457.004.png
 
RUTHI
wewe ni mwanamke mwenye tabia nzuri.
12 Ingawa ni kweli kwamba mimi ndiye jamaa
aliye karibu, lakini kuna mtu mwingine wa jamaa
aliye karibu zaidi wa kukomboa kuliko mimi.
13 Wewe kaa hapa usiku huu, kisha asubuhi
kama akikubali kukomboa, vema na akomboe.
La sivyo kama hayuko tayari, hakika kama
BWANA aishivyo nitafanya hivyo. Lala hapa
mpaka asubuhi.’’
5 Ndipo Boazi akasema “Siku utakaponunua
shamba kutoka kwa Naomi na Ruthi Mmoabi,
itakubidi kumchukua pia huyo mjane, ili
kudumisha jina la marehemu pamoja na mali
yake.”
6 Kuhusu hili, yule jamaa wa karibu wa
kukomboa akasema, “Basi mimi sitaweza
kukomboa kwa sababu inaonekana
nitauhatarisha urithi wangu. Wewe komboa
mwenyewe. Mimi sitaweza.”
7 (Basi katika siku za kale huko Israeli, ili
kukamilisha tendo la kukomboa na kukabidhiana
mali, mmoja huvua kiatu chake na kumpatia
mwingine. Hii ilikuwa ni njia ya kuhalalisha
mabadilishano katika Israeli.)
8 Basi yule jamaa wa karibu wa kukomboa
akamwambia Boazi, “Wewe nunua mwenyewe.’’
Naye huyo jamaa akavua kiatu chake.
9 Kisha Boazi akawatangazia wazee na watu
wote waliokuwepo, “Leo ninyi ni mashahidi
kwamba mimi nimenunua kutoka kwa Naomi
yote yaliyokuwa mali ya Elimeleki, Kilioni na
Maloni. 10 Nimemchukua pia Ruthi Mmoabi,
mjane wa Maloni, awe mke wangu, ili
kuendeleza jina la marehemu pamoja na mali
zake, ili jina lake marehemu lisitoweke miongoni
mwa jamaa yake wala katika kumbukumbu za
mji wake. Leo hivi ninyi ni mashahidi!”
11 Kisha wazee pamoja na watu wote
waliokuwa langoni wakasema, “Sisi ni
mashahidi. BWANA na amfanye mwanamke
huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama
Raheli na kama Lea, wale wawili ambao kwa
pamoja waliijenga nyumba ya Israeli. Nawe
ufanikiwe katika Efrata, na uwe mashuhuri katika
Bethlehemu. 12 Kupitia kwa watoto ambao
BWANA atakupa kutokana na huyu mwanamke
kijana, jamaa yako na ifanane na ya Peresi,
ambaye Tamari alimzalia Yuda.”
14 Hivyo huyo mwanamke akalala miguuni
pake mpaka asubuhi, akaondoka mapema
asijaweza mtu kumtambua mwenzake, maana
Boazi alisema, “Isijulikane kabisa ya kuwa
mwanamke alifika kwenye sakafu ya kupuria.”
15 Pia akamwambia, “Lete shela yako
uliyoivaa uitandaze.” Naye alipoitandaza,
akamimina vipimo sit a a vya shayiri akamtwika.
Kisha Ruthi akarudi zake mjini.
16 Basi Ruthi alipofika kwa mama mkwe
wake Naomi, akamwuliza, “Je, binti yangu,
ilikuwaje huko?
Ndipo akamwelezea kila kitu Boazi
alichomfanyia. 17 Akaendelea kusema, “Amenipa
shayiri vipimo sita akisema, ‘Usiende kwa mama
mkwe wako mikono mitupu.’ ”
18 Kisha Naomi akasema, “Subiri binti yangu,
mpaka utakapojua kwamba hili jambo
limekwendaje. Kwa sababu mtu huyu hatatulia
mpaka akamilishe jambo hili leo.”
Boazi Amwoa Ruthi
Boazi akakwea mpaka kwenye lango la
mji, akaketi pale. Kisha muda si mrefu
yule mtu wa jamaa aliyekuwa wa karibu wa
kukomboa, ambaye Boazi alimtaja, akaja. Boazi
akasema, “Njoo hapa rafiki yangu, karibu uketi.”
Naye akakaribia, akaketi.
2 Boazi akatwaa watu kumi miongoni mwa
wazee wa mji, akawaambia, “Ketini hapa.” Nao
wakaketi. 3 Kisha akamwambia yule jamaa wa
karibu wa kukomboa, “Huyu Naomi, aliyerudi
hapa kutoka nchi ya Moabu, anauza sehemu ya
ardhi iliyokuwa mali ya ndugu yetu Elimeleki.
4 Nami niliwaza nikujulishe wewe na kukuambia
uinunue mbele ya hawa waliopo hapa na mbele
ya wazee wa watu wangu. Kama wewe
utaikomboa, haya fanya hivyo. Lakini kama
hutaikomboa, uniambie, ili nijue. Kwa kuwa
hakuna mtu mwingine mwenye haki ya
kuikomboa ila wewe na baada yako ni mimi.”
4
Wazao wa Boazi
13 Basi Boazi akamwoa Ruthi, naye akawa
mke wake. Alipoingia kwake, BWANA akamjalia
Ruthi naye akapata mimba, akamzaa mtoto wa
kiume. 14 Wanawake wakamwambia Naomi:
“Ahimidiwe BWANA, asiyekuacha bila kuwa na
jamaa wa karibu wa kukomboa. Na awe
mashuhuri katika Israeli yote! 15 Atakurejeshea
uhai wako na kukuangalia katika siku za uzee
wako. Kwa maana mkweo ambaye anakupenda
na ambaye kwako ni bora zaidi ya watoto wa
kiume saba, ndiye aliyemzaa.’’
Naye akasema, “Nitaikomboa mimi.”
a 15 Vipimo sita hapa ni sawa na kilo 15, pia mstari wa 17
4
952102457.001.png
 
RUTHI
16 Basi Naomi akamchukua yule mtoto,
akampakata na akawa mlezi wake. 17 Wanawake
waliokuwa jirani zake, wakasema, “Naomi ana
mtoto wa kiume.” Wakamwita jina lake Obedi.
Yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake
Daudi.
18 Hivi ndivyo vizazi vya Peresi:
Peresi alimzaa Hesroni,
19 Hesroni akamzaa Ramu,
Ramu akamzaa Aminadabu,
20 Aminadabu akamzaa Nashoni,
Nashoni akamzaa Salmoni;
21 Salmoni akamzaa Boazi,
Boazi akamzaa Obedi;
22 Obedi akamzaa Yese
na Yese akamzaa Daudi.
5
952102457.002.png
 
Zgłoś jeśli naruszono regulamin