TI_Kiswahili_1068.pdf

(35 KB) Pobierz
Tito
Utangulizi
Waraka huu aliandikiwa Tito mmoja wa wafuasi wa Paulo muda mfupi tu baada ya Paulo kumwachia wajibu
wa kuangalia na kuimarisha kanisa huko Krete. Tito alikuwa na wajibu wa kuwaweka wazee wa kanisa,
kuwasimika na kuwafundisha kushika misingi ya imani ya Kikristo. Inaonekana kwamba Paulo alikuwa Korintho
akiwa njiani kwenda Nikopoli huko Akaya (3:12). Waraka huu umeandikwa baada ya kuachiwa kutoka gerezani
Rumi mara ya kwanza, huenda kati ya 63B.K. na 65 B.K.
Waraka huu unaonyesha kuwa kanisa huko Krete halikuwa na mpangilio na kwamba lilikuwa na washirika
waliohitaji maelekezo mahsusi. Ilimbidi Paulo aeleze kwa kina kuhusu sifa za wazee wa kanisa na pia kutoa
mafundisho kadha wa kadha kwa waamini wengine pia. Katika mafundisho hayo, Paulo anagusia juu ya matatizo
yanayowapata watumishi wa Mungu na jinsi matatizo hayo yanavyoweza kutatuliwa.
Tito alikuwa mshirika wa Paulo kwa karibu muda wa miaka kumi na mitano.Akiwa mwongofu Mmataifa
kutoka Antiokia na kama mwamini asiyetahiriwa, alifuatana na Paulo na Barnaba kwenda kwenye baraza la
Yerusalemu (Gal.2:1-3 ). Aliendelea kusafiri na Paulo ( ona 2Kor.2:12 – 13:7;5 – 7:13-14; 8:3,16-17), hivyo Paulo
akawa amemwacha huko Krete.
Wazo Kuu
Mkazo wa barua hii ni kuhusu umuhimu wa kuishi maisha matakatifu katika Kristo katikati ya uovu ulioko
duniani. Ingawa katika maisha yetu duniani tunazungukwa na uovu na chuki, hatuna budi maisha yetu kuwa
kielelezo jinsi neema ya Mungu inavyotupatia ushindi. Maisha kama hayo yataleta matokeo mema. Paulo
anarudia mara kwa mara kusisitiza juu ya kudumisha matendo mema. Maneno matupu hayawezi kufanya lo lote,
inatubidi tuishi maisha yenye matendo mema.
Katika waraka huu, Mtume Paulo anakaribia sana kuweka ukiri wa imani katika uandishi wake wote.Vidokezo
muhimu vya MAFUNDISHO (THEOLOGIA ) ya Agano Jipya vinaonekana katika waraka huu.
Mgawanyo
Salamu (1:1-4)2
Sifa za wazee wa kanisa (1:5-16) 3
Maelezo ya jumla kuhusu waamini (2:1-15)4
Maagizo kuhusu maisha yawapasayo wakristo (3:1-15).
1
Tito
wapate kuwa wazima katika imani, 14 ili
wasiendelee kuangalia hadithi za Kiyahudi au
maagizo ya wale watu wanaoikataa kweli.
15 Kwa wale walio safi, kila kitu ni safi kwao.
Lakini kwa wale waliopotoka na wasioamini,
hakuna cho chote kilicho safi. Kwa kweli nia zao
na dhamiri zao zimepotoka. 16 Wanadai kumjua
Mungu, lakini kwa matendo yao wanamkana.
Hao watu ni chukizo, wasiotii, wasiofaa kwa
jambo lo lote jema.
Salamu
Paulo, mtumishi wa Mungu na mtume wa
Yesu Kristo kwa ajili ya imani ya wateule
wa Mungu na ujuzi wa kweli ile iletayo uchaji wa
Mungu, 2 imani na ujuzi ulioko katika tumaini la
uzima wa milele ambao Mungu,asiyesema
uongo, aliahidi hata kabla ya kuwekwa misingi
ya ulimwengu, 3 Naye kwa wakati Wake
aliouweka alilidhihirisha neno Lake kwa njia ya
mahubiri ambayo mimi nimewekewa amana
kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu.
1
Fundisha Mafundisho Manyofu
Lakini kwa habari yako wewe, inakupasa
kufundisha kulingana na mafundisho
yenye uzima. 2 Wafundishe wazee kuwa na
kiasi, wastahivu, wenye busara na wanyofu
katika imani, upendo na saburi.
3 Vivyo hivyo wafundishe wanawake wazee
kuwa na mwenendo wa unyenyekevu
unaostahili utakatifu, wala wasiwe wasingiziaji
au walevi, bali wafundishe yale yaliyo mema, 4 ili
waweze kuwafundisha wanawake vijana kuwa
na kiasi, wawapende waume zao na kuwapenda
watoto wao, 5 wawe waaminifu, watakatifu,
wakitunza vema nyumba zao, wema, watiifu
kwa waume zao, ili mtu ye yote asije akalikufuru
neno la Mungu.
6 Vivyo hivyo, sisitiza vijana kuwa na kiasi.
7 Katika kila jambo wewe mwenyewe uwe
kielelezo cha matendo mema na katika
mafundisho yako uonyeshe unyofu, utaratibu,
ukweli 8 na maneno yenye uzima, yale ambayo
hayawezi kulaumiwa, hata wale wenye
kukupinga watahayari, wakose neno lo lote
baya la kusema juu yetu.
9 Wafundishe watumwa kuwatii mabwana
zao katika kila jambo, wakijitahidi kuwapendeza
wala wasijibizane nao, 10 wala wasiwaibie, bali
watumwa waonyeshe kuwa wanaweza
kuaminika kabisa, ili kwamba kwa kila namna
wayafanye mafundisho ya Mungu Mwokozi wetu
kuwa ya kupendeza.
11 Kwa maana neema ya Mungu iwaokoayo
wanadamu wote imefunuliwa. 12 Nayo
yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za
kidunia, ili tupate kuishi maisha ya kiasi, ya haki
na ya kumcha Mungu, katika ulimwengu huu wa
sasa, huku 13 tukilitazamia tumaini lenye baraka
na ufunuo wa utukufu wa Mungu wetu Mkuu na
Mwokozi wetu Yesu Kristo, 14 Yeye ndiye
aliyejitoa nafsi Yake kwa ajili yetu ili atukomboe
kutoka katika uovu wote na kujisafishia watu
kuwa mali Yake Mwenyewe, yaani, wale walio
2
4 Kwa Tito, mwanangu mwaminifu katika
imani tunayoshiriki sote.
Neema iwe kwako na amani itokayo kwa
Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Mwokozi
wetu.
Kazi Ya Tito Huko Krete
5 Sababu ya mimi kukuacha huko Krete ni ili
uweke kwenye utaratibu mambo yale yaliyosalia
na kuwaweka wazee wa kanisa katika kila mji,
kama nilivyokuagiza. 6 Mzee wa kanisa asiwe na
lawama, awe mume wa mke mmoja, mtu
ambaye watoto wake ni waaminio na wala
hawashtakiwi kwa ufisadi. 7 Kwa kuwa askofu,
kama wakili wa Mungu, imempasa kuwa mtu
asiye na lawama, asiwe mwenye majivuno au
mwepesi wa hasira, wala mlevi, wala asiwe mtu
mwenye tamaa ya mapato yasiyo ya halali. 8 Bali
awe mkarimu, anayependa mema, mwenye
kiasi, mwenye haki, mwadilifu, mnyofu,
mtakatifu na mwenye kuitawala nafsi yake.
9 Inampasa alishike kwa uthabiti lile neno la
imani kama lilivyofundishwa, kusudi aweze
kuwafundisha wengine kwa mafundisho
manyofu na kuwakanusha wale wanaopingana
nayo.
Walimu Wa Uongo
10 Kwa maana wako wengi wasiotii, wenye
maneno yasiyo na maana, hasa wale wa kikundi
cha tohara. 11 Hao ni lazima wanyamazishwe,
kwa sababu wanaharibu watu wa nyumba
nzima wakifundisha mambo yasiyowapasa
kufundisha. Wanafanya hivyo kwa ajili ya
kujipatia mapato ya udanganyifu. 12 Hata
mmojawapo wa manabii wao mwenyewe
amesema: ‘‘Wakrete ni waongo sikuzote,
wanyama wabaya, walafi, wavivu.’’ 13 Ushuhuda
huu ni kweli. Kwa hiyo, uwakemee kwa ukali
2
952117969.001.png
 
Tito
na bidii katika kutenda mema.
15 Basi wewe fundisha mambo haya, onya
na karipia kwa mamlaka yote. Mtu ye yote
asikudharau.
matunda.
15 Wote walio pamoja nami wanakusalimu.
Wasalimu wale wanaotupenda katika imani.
Neema iwe nanyi nyote. Amen.
Kutenda Mema
Wakumbushe watu kuwanyenyekea
watawala na kuwatii wenye mamlaka,
wawe tayari kutenda kila lililo jema.
2 Wasimnenee mtu ye yote mabaya, wasiwe
wagomvi, bali wawe wapole, wakionyesha
unyenyekevu kwa watu wote.
3 Maana sisi wenyewe wakati fulani tulikuwa
wajinga, wasiotii, tukiwa watumwa wa tamaa
mbaya na anasa za kila aina. Tuliishi katika
uovu na wivu, tukichukiwa na kuchukiana sisi
kwa sisi. 4 Lakini wema na upendo wa Mungu
Mwokozi wetu ulipofunuliwa, 5 alituokoa, si kwa
sababu ya matendo ya haki tuliyotenda, bali
kwa sababu ya rehema Zake. Alituokoa kwa
kutuosha, kwa kuzaliwa mara ya pili na kwa
kufanywa wapya kwa njia ya Roho Mtakatifu,
6 ambaye Mungu alitumiminia kwa wingi kwa njia
ya Yesu Kristo Mwokozi wetu, 7 ili kwamba,
tukiisha kuhesabiwa haki kwa neema Yake,
tupate kuwa warithi tukiwa na tumaini la uzima
wa milele. 8 Hili ni neno la kuaminiwa. Nami
nataka uyasisitize mambo haya, ili wale ambao
wamemwamini Mungu wapate kuwa waangalifu
kujitoa kwa ajili ya kutenda mema wakati wote.
Mambo haya ni mazuri tena ya manufaa kwa
kila mtu.
9 Lakini jiepushe na maswali ya kipuzi,
mambo ya koo, mabishano na ugomvi kuhusu
sheria, kwa sababu haya hayana faida tena ni
ubatili. 10 Mtu anayesababisha mafarakano,
mwonye mara ya kwanza, kisha mwonye mara
ya pili. Baada ya hapo, usihusike naye tena.
11 Kwa kuwa unajua kwamba mtu kama huyo
amepotoka na tena ni mwenye dhambi. Yeye
amejihukumu mwenyewe.
3
Maneno Ya Mwisho Na Kumtamkia Baraka
12 Mara nitakapomtuma Artema au Tikiko
kwako, jitahidi kuja unione huko Nikopoli, kwa
sababu nimeamua kukaa huko wakati wa majira
ya baridi. 13 Fanya kila uwezalo uwasafirishe
Zena, yule mwanasheria na Apolo na
uhakikishe kwamba wana kila kitu
wanachohitaji. 14 Watu wetu hawana budi
kujifunza kujitoa kutenda mema, ili waweze
kuwasaidia watu wenye mahitaji ya lazima ya
kila siku, wasije wakaishi maisha yasiyokuwa na
3
952117969.002.png
 
Zgłoś jeśli naruszono regulamin